You are currently viewing Dondoo muhimu sana kwa wazazi na walezi watarajiwa

Dondoo muhimu sana kwa wazazi na walezi watarajiwa

Zifuatazo ni dondoo 8 za msingi kwa wazazi, walezi ama watalajiwa katika kuimalisha na kudumisha malezi bora kwa mtoto.

  1. Mkanye mtoto wako wa kike kuhusu kukubali kupakatwa hovyo, bila kujali ni nani anampakata, hata kama ni mjomba wake.
  2. Usivue nguo mbele ya mwanao pindi akifikisha miaka 2 au zaidi. Jifunze kumwomba akupishe
  3. Usiruhusu mtu yoyote amwite mwanao “Mchumba”, “Mke wangu” au “Mme wangu”.
  4. Kila wakati mwanao anapoenda kucheza na wenzake, hakikisha unafuatilia kujua wanacheza nini, siku hizi hata watoto wanafundishana michezo michafu.
  5. Kama mwanao ameonyesha kutopenda kwenda mtu fulani usimlazimishe, pia chunguza kwa ukaribu ili kujua sababu.
  6. Inashauriwa kupitia kwanza mwenyewe movie yoyote kabla ya kuruhusu mwanao waiangalie.
  7. Mwanao anapofikisha umri wa miaka 3 anza kumfundisha jinsi ya kusafisha sehemu zake za siri mwenyewe, na umuonye asiruhusu mtu yoyote kumshika sehemu hizo.
  8. Mfundishe mwanao thamani ya kuishi bila kufuata mkumbo.Mwanao akilalamika kuhusu mtu fulani, usikae kimya.

Toa Jibu