Karibu Sana

KILA MTOTO ANAHESABIKA

Kupitia Taasisi yetu, tumedhamiria kujenga mustakabali salama kwa watoto wetu na kuzuia machungu ya kupoteza watoto.

Pamoja, tuungane kufanikisha lengo hili. Je, unaweza kujiunga nasi katika jitihada hizi?

Tunachokifanya

Pamoja tunaweza kuleta mabadiliko.

Shirika letu linatambua kuwa suala la watoto kupotea ni changamoto ngumu na lenye sura nyingi, linalohitaji mbinu za kitaalamu katika kukabiliana nalo.

Kupitia msaada wetu endelevu kwa watoto, familia, na jamii, na kwa kushirikiana na mashirika mengine, pamoja tunafanikisha jitihada zetu za kuhamasisha na kuongeza uelewa, huku lengo letu kuu ni kupunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya watoto wanaopotea nchini Tanzania.

Hatua za haraka na za ushirikiano ni muhimu sana katika kuwatafuta na kuwarejesha watoto waliopotea.

Usaidizi wa ushauri nasaha na huduma nyinginezo unaweza kuwasaidia watoto na familia kuhimili athari za kihisia na kupona kutokana na tukio la upotevu wa mtoto.

Lengo letu ni kuunda dhamira na wajibu katika jamii ili kuzuia na kutafuta watoto waliopotea.

Lengo letu ni kulinda maisha ya watoto walio katika mazingira hatarishi kwa kutumia utafiti, kuhamasisha mabadiliko ya sera, na kukuza mazoea bora.

Wafahamu watoto waliopotea

Ikiwa umewaona watoto hawa au unajua walipo, tafadhali usisite  kuwasiliana nasi mara moja.

Unahofu ya kumpoteza mtoto?

Jifunze mbinu za kumlinda mtoto wako na hatua za kuchukua endapo utagundua kuwa ametoweka.

Tusaidie kuchukua hatua

Kwa kushiriki, unaweza kuleta mabadiliko makubwa na chanya katika maisha ya watoto wetu.

Taarifa za Watoto

Tusaidie kuwatambua watoto waliopotea na kupatikana.

Jiunge na Harakati

Kila mwaka, watoto wengi hupotea, na kuacha familia zenye majonzi na jamii zenye majeraha. Lakini kwa msaada wako, tunaweza kubadilisha hali hii. Kuna njia nyingi za kushiriki na kuwa sehemu ya suluhisho—kuanzia kujitolea muda wako hadi kutoa michango ya aina mbalimbali.

Jiunge nasi leo ili tuweze kuwa sehemu ya mabadiliko.

Uhalisia Wakushtusha Kuhusu

Maonyesho ya
Biashara ya Sabasaba

Maonyesho haya, yanayofanyika kila mwaka katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, kitovu cha uchumi wa Tanzania, ni jukwaa muhimu kwa wafanyabiashara kuonyesha bidhaa na huduma zao. Maonyesho haya huvutia umati mkubwa wa watu, hali inayoweza kuleta changamoto kwa wazazi na walezi katika kuhakikisha watoto wao wako salama. Katika mazingira yenye pilikapilika nyingi, kuna hatari ya watoto kupotea au kuachwa nyuma, jambo linaloongeza uwezekano wa kutengana na familia zao. Kutokuwepo kwa mfumo wa haraka na bora wa kutambua na kuwasaidia watoto waliopotea kurudi kwa familia zao kunaongeza ukubwa wa tatizo hili.

Kila mtoto ni wa thamani!

Tunahitaji msaada wako ili kutoa mchango halisi katika mapambano dhidi ya tatizo la watoto kupotea nchini Tanzania. Mchango wako unaweza kusaidia kufadhili programu na mipango muhimu ya kuzuia watoto kupotea, kutoa elimu kwa jamii na watoto kuhusu usalama, na kuhakikisha kuwa kuna majibu ya haraka na yenye ufanisi yanapohitajika mara watoto wanapopotea.

Kama wazazi, tunajua jinsi ilivyo muhimu kuwalinda watoto wetu. Kwa bahati mbaya, watoto wengi huenda wanapotea na kuwa hatarini.

Kama jamii, tunaweza kushirikiana na kutumia teknolojia ya kisasa ili kuwasaidia watoto wetu kurejea nyumbani.

Saliboko Hassan

Dar es Salaam, Tanzania

Soma Kuhusu