UTANGULIZI

Wapo Wapi App

Kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto wanaopotea na changamoto zinazohusiana na mbinu za kuwapata kwa haraka na kwa ufanisi. Mifumo ya sasa ya kuripoti na kusambaza habari kuhusu watoto waliopotea mara nyingi ina changamoto zinazochelewesha mchakato wa utafutaji na upatikanaji wao, na hakuna kumbukumbu ya kanzidata inayopatikana kwa urahisi.

Aidha, ukosefu wa mfumo jumuishi na rahisi wa kuzuia, kuripoti, na kushiriki habari kuhusu watoto wanaopotea unafanya iwe changamoto kwa umma, vyombo vya usalama, na wadau wanaotoa msaada kushirikiana kwa ufanisi katika kuwapata watoto.

Programu ya kwanza ya bure na rahisi kutumia nchini Tanzania inalenga kupunguza idadi ya watoto wanaopotea na kusaidia katika kuwapata kwa kutoa taarifa muhimu, rasilimali, tahadhari, na tarifa kwa watumiaji. Programu hii pia inawaruhusu watumiaji kuripoti matukio ya kuonekano au kutoa vidokezo, hivyo kuwawezesha watu wote kushirikiana kwa urahisi katika kuzuia na kuwasaka watoto waliopotea.

Mikinzano ya Hoja

Hoja ya 1

Kuna zaidi ya mashirika 30 yasiyo ya serikali ya ndani na kimataifa yanayofanya kazi nchini Tanzania yanayolenga watoto, lakini hakuna hata moja inayojishughulisha sana na suala la upotevu wa watoto.

Hoja ya 2

Zaidi ya programu 30,000 zinapatikana kwenye App Store na Google Playstore kwa watumiaji wa mtandao nchini Tanzania. Hata hivyo, hakuna programu kati ya hizi inalenga kupunguza idadi ya watoto wanaopotea au kusaidia katika kupatikana kwa watoto.

Vipengele vya Kipekee

Baadhi ya vipengele vilivyomo ni;

Ripoti ya watoto waliopotea

Kupitia programu hii, watumiaji wataweza kwa urahisi kupata taarifa kamili kuhusu watoto waliopotea, ikiwa ni pamoja na majina yao, picha zao za sasa, maelezo ya kina kuhusu sifa zao, na taarifa muhimu nyinginezo.

Vidokezo vya Kiusalama na Rasilimali

Programu hii inatoa vidokezo vya kiusalama na rasilimali kwa wazazi na walezi ili kusaidia kuzuia ongezeko la upotevu wa watoto, ikiwa ni pamoja na ushauri kuhusu usalama wa watoto, hatua za tahadhari, na nini cha kufanya iwapo mtoto atapotea.

Onyo & Taarifa

Programu hii inatoa vidokezo vya kiusalama na rasilimali kwa wazazi na walezi ili kusaidia kuzuia ongezeko la upotevu wa watoto, ikiwa ni pamoja na ushauri kuhusu usalama wa watoto, hatua za tahadhari, na nini cha kufanya iwapo mtoto atapotea.

Zana ya utoaji Taarifa

Muundo wa programu unaovutia na maelekezo yake yapo wazi na kufanya iwe rahisi kwa mtu yeyote kuripoti mtoto aliyepotea, pamoja na taarifa za kuonekano au taarifa nyingine muhimu zinazoweza kusaidia katika kupaapata au kuzuia kupotea kwa watoto.

Tafuta & Vichujio

Programu hii ina uwezo wa kutafuta na kuchuja ili kupitia kanzidata ya watoto waliopotea na orodha nyingine za taarifa muhimu kwa urahisi. Hii inawasaidia watumiaji kupata taarifa zinazolingana na vigezo wanavyotafuta.

Unganishaji wa Mitandao ya Kijamii

Kwa kujumuisha majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii, programu inaweza kufikia hadhira kubwa zaidi na kuwezesha kuongezeka kwa nafasi za kupunguza, kuwapata watoto waliopotea na ugawaji wa rasilimali.